Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha wanaliangalia upya suala la Wahadhiri ili waweze kuendelea kufundisha hata baada ya kutimiza miaka 65.

Dkt. Tulia amesema hayo Bungeni leo Juni 14, 2021, mara baada ya mbunge wa viti maalum Dkt. Thea Ntare kuibua mjadala wa uhaba mkubwa wa Wahadhiri nchini.

Ambapo serikali ilisema kuwa itahakikisha inaangalia namna bora ya kurekebisha sheria hizo ili kuendana na uhitaji wa sasa wa soko la Wahadhiri nchini.

“Naibu Waziri hili mkalitazame kwa sababu mtu anapofikisha miaka 65 ndiyo amebobea kwenye eneo lake, sasa ukimuondoa huyo ukasema unatengeneza ajira mpya hakuna uhalisia, kwa sababu unayemuajiri haweza kuwa kama huyo mwenye miaka 65, kuna Maprofesa wengine hawana kazi za kufanya lakini wamestaafu na vichwa vyao viko sawa sawa wanaweza kuendelea kufanya kazi,” amesema Dkt. Tulia.

Biden kuzungumza na viongozi wa nchi 3 za Baltic
Wizi wa mafuta wakithiri Kigamboni,15 wakamatwa