Ofisi ya Uhamiaji Mkoani Njombe imekamata wahamiaji haramu 12 kutoka nchi za Rwanda, Somalia na Burundi wakitokea mkoani Dodoma kuelekea Tunduma mkoani Songwe kwa lengo la kwenda Afrika Kusini kutafta maisha.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Njombe, Abbas Missana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wahamiaji hao saba ni raia wa Rwanda, wawili ni raia wa Burundi na watatu ni kutoka Somalia.

“Wahamiaji hawa wote kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani Dodoma na walikuwa wakisafiri kwa mabasi ya SATCO, SUPER FEO na SHABIBY wakielekea Tunduma hadi Zambia na Afrika ya Kusini kwa ajili ya kutafuta maisha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa taarifa kwa mtu yeyote ambaye una mashaka na uraia wake hapa Tanzania toa taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,”amesema Missana

Aidha, amesema kuwa wote waliokamatwa Idara inakusudia kuwafikisha mahakani na kuwafungulia mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria na kuwataka wananchi kuwa na mapenzi na nchi yao huku akisisitiza kutoa taarifa kwenye vyombo husika pindi anapoonekana mtu yeyote anayetiliwa mashaka.

Baadhi ya wananchi mjini Njombe wamesema kuwa Watanzani wamekuwa na tabia ya wema licha ya kukubali wito wa ofisa uhamiaji huku wakiiomba Idara ya Uhamiaji mkoani Njombe kuendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuelewa sehemu sahihi ya kuwapeleka.

  • Ziara ya Rais Magufuli mkoani Dodoma
  • Fahamu visababishi vya mshituko wa moyo, kiharusi
  • Lema kifungoni hadi mwaka 2020

Utoro watajwa kushusha kiwango cha ufaulu shule ya msingi Itulike mjini Njombe
Video: Tazama video nzima wimbo wa baba yake Diamond ''Dudulayoyo''