Raia sita wa Malawi walioingia nchini bila kibali wamekamatwa Kibaha mkoani Pwani wakiwa safarini kwenda jijini Dar es Salaam kutafuta kazi ya kuuza baa au kusuka mitindo mbalimbali ya nywele kwenye saluni.

Raia hao wamekamatwa eneo la Tanita mjini Kibaha wakiwa kwenye gari aina ya Toyota  Hiace.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema, walipowahoji raia hao wamesema wanatoka mkoani Mbeya na wanaenda kutafuta kazi kwenye baa na saluni ili wapate fedha za kuendesha maisha yao.

Ameongeza kuwa dereva wa gari hilo (jina limehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi) anashikiliwa kwa kosa la kuwasafirisha wahamiaji hao.

Kamanda Nyigesa ametoa onyo kwa madereva na watu wenye tabia ya kusafirisha wahamiaji haramu kuacha mara moja biashara hiyo.

KMC FC: Hatuna hofu na Mwadui FC
Nugaz awatuliza Young Africans