Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mkoa wa Lindi upo hatarini kugeuka jangwa na tayari vyanzo vingi vya maji vimeanza kukauka kwa sababu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na watu kufanya shughuli za kijamii kwenye vyanzo vya maji.

Kufuatia hali hiyo hatarishi, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Mkoa huo kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaoharibu mazingira kwa kufyeka na kuchoma moto misitu kwa sababu wanaharibu mazingira na kusababisha ukame.

Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Nanjaru, Nachinyimba, Nambiranje, Mkaranga, Nandenje, Nachinyimba na Mandarawe Oktoba 18, 2016, ambapo amewaeleza wakulima wa ufuta kuwa wanatakiwa kuendelea kutumia mashamba yao ya zamani na kuacha tabia ya kufyeka misitu kila mwaka na badala yake waanzishe mpango wa upandaji miti ili kuepusha taifa kugeuka kuwa jangwa.

Majaliwa amesema vyanzo vya maji vimekauka kwa sababu miti mingi imekatwa, Mito yote iliyokuwa inatiririsha maji imekauka. Hivyo amewataka viongozi wa mkoa kuhakikisha misitu inalindwa na atakayekutwa analima kwenye vyanzo vya maji akamatwe kwani ukataji miti unaoendelea katika maeneo hayo hakutosababisha kukosekana kwa maji tu, bali  hata mazao yatapungua na sababisha njaa katika vijiji vyetu.

Amesema kwa sasa Serikari inatumia gharama kubwa kuchimba visima virefu kutafuta maji. Amesema zamani walikuwa wanachimba mita 20 au 30 wanakuta maji na gharama yake ilikuwa sh. milioni 35, ambako kwa sasa wanalazimika kuchimba mita zaidi ya 150 kwa gharama y ash milioni 75 kwa kisima kimoja.

 

Ronaldo de Lima Amfagilia Cristiano Ronaldo
Masauni afanya mazungumzo na wajumbe kutoka UNDP