Ili wanawakwe wengi waweze kushika nafasi za Uongozi, Waandishi wa Habari wanawajibu wa kuripoti habari zitakazowaibua katika shughuli mbalimbali kwa minajili ya kuchochea uwajibikaji kwa maslahi ya Umma.

Rai hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa wakati akiongea na waandishi wa habari vijana wanaoendelea kupatiwa mafunzo maalumu ya kujengewa uwezo juu ya kuripoti habari za wanawake kushika nafasi za uongozi.

Mwenyekiti wa Jumuia ya changamoto zinazowakabili wajane Zanzibar (ZAWIO), Tabia Makame akizungumzia kuhusu uzoefu wa kazi kwa waandishi wa habari vijana.

Amesema kwa muda mrefu wanawake wengi wamekua wakishindwa kufikia malengo ya kushika nafasi za uongozi, kutokana na dhana potofu ya kuamini wanaume pekee ndio wenye dhamana jambo ambalo linapingwa na mikataba yote ya kikanda na kimataifa.

Kwa upande wake mmoja wa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Fatma Aloo akizungumzia harakati mbali mbali alizopitia za kuazisha chama hicho mwaka 1987 amesema wakati wanaanza harakati hizo walipewa majina mengi lakini hawakukata na waliangalia wanawezaje kufikia malengo yao.

Serikali kuishirikisha jamii faida Bima ya Afya kwa wote
Papa Francis kuzulu DRC huku hofu ya M23 ikizidi kutawala