Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mwanaidi Ally amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango kampasi ya Mwanza kuhakikisha wanajiajiri.

Mwanaidi amesema serikali imetenga fedha za mikopo pamoja na kupunguza riba katika mikopo ilivijana waweze kujiajiri kupitia vikundi au kujiajiri binafsi.

Rai hiyo ameitoa wakati wa mahafali ya 34 ya Chuo hicho na kuongeza kuwa serikali imeweka mipangomizuri kwa kutoa fursa kwa vijana.

Ameziagiza za Taasisi za Elimu ya juu nchini kuhakikisha zinatumia vyema vyanzo vya mapato naasilimia 10 ya bajeti yao inatakiwa iwe inatokana na vyanzo vya miradi ya taasisi husika na kukitakachuo hicho kuhakikisha kinatekeleza miradi ya chuo chao katika kuinua uchumi.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mipango kampasi ya Mwanza, Profesa Hozen Mayaya alisema Chuo chaokimeboresha mazingira ya kufundishia na kuwa chuo chao kimefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mrefuna kimefanikiwa kuongeza udahili kutoka wanafunzi 406 mwaka 2015/2016 na mwaka huu inawanafunzi 4,095.

Mwaka huu wamehitimu wanafunzi 2,571 katika ngazi ya Stashada, Astashahada na Shahada.Wanaume wakiwa ni 1009 na wanawake 1,562

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 11, 2021
‘Ninamtafuta Lowasa’