Naibu Waziri wa Afya nchini Iran, Qassem Janbabaei, jana ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Virusi vya corona vimewaathiri wahudumu wa afya wapatao 10,000 nchini humo,

Ripoti za mapema wiki hii, zimesema idadi ya wafanyakazi wa huduma ya afya walioambukizwa virusi hivyo ni 800 tu.

Iran imesema zaidi ya watu 100 miongoni mwa wa wafanyakazi hao wamefariki dunia.

Imeelezwa kuwa Iran ni taifa la Mashariki ya Kati linalokabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa virusi vya corona, ambapo takriban watu 7,249 wamepoteza maisha kati ya watu 129,000 waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Takwimu hizo ni pamoja na vifo zaidi ya 66 vilivyotangazwa jana Alhamisi na msemaji wa Wizara ya Afya Kianoush Jahanpour.

Ligi kuchezwa Dar es salaam, Mwanza
Burundi watakiwa kuwa watulivu, matokeo wiki ijayo