Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imewahukumu watu watatu  kifungo cha miaka 73 jele kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuua tembo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Ngaile wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti, amesema adhabu hiyo imetolewa  kutokana na kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo ya jela ni Augen Nicodemus, Mwita Marwa na Amos Alexander wote wakazi wa Wilaya ya Serengeti.

Aidha, Hakimu Ngaile amesema kuwa katika kosa la kwanza la kuingia na silaha ndani ya hifadhi kinyume ch sheria za nchi kwaajili  ya kufanya vitendo vya ujangili, mahakama imewahukumu watumikie adhabu ya miaka 15 jele  kila mmoja.

Ngaile ameongeza kuwa kosa la pili  ni la kusafirisha silaha kutoka Burundi  hadi Tanzania kinyume cha kifungu namaba 18 cha Sheria ya mlipuko  ya mwaka 2002 ambapo walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Katika kosa la tatu la kupatikana na silaha ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kinyume cha sheria ya Hifadhi ya Taifa ya mwaka 2002 watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja, ameongeza kuwa katika kosa la nne la kuingia kwenye Hifadhi bila kibali washtakiwa watatumikia kifungo cha mwaka mmoja kila mmoja, na kosa la tano la kuuwa Tembo ndani ya hifadhi adhabu yake ni miaka 10.

Hata hivyo amesema kuwa katika kosa la sita la kupatikana na nyara za Serikali kinyume cha Sheria ya wanyama pori namba tano ya mwaka 2009 washtakiwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Nyota Watatu Wajiunga Rasmi Azam FC
Vigogo TRA kizimbani kwa rushwa ya milion 66/-