Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema baadhi ya mashambulizi yanayotokea katika eneo la kusini mwa  Tanzania mpakani na Msumbiji yanafanywa na vijana waliotoroka Tanzania baada ya kufanya vitendo kama hivyo katika mikoa ya Pwani na Tanga.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo katika Jeshi la Polisi Tanzania, Liberatus Sabas amesema kwamba baadhi ya vijana hao walitoroka shule na kujiunga na makundi hayo.

Amesema  licha ya matukio hayo ya mashambulizi kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa, jamii ya Watanzania inatakiwa kufuatialia kwa karibu  mienendo ya vijana katika jamii ili kukomesha hali ya vijana kujiunga na makundi ya uhalifu.

Sabas ameongeza kuwa polisi nchini imewakamata watu kadhaa kwa ushirikiano wa maafisa wa usalama wa Msumbiji, wakihusishwa na  mashambulizi hayo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 24, 2020
Israel yaitisha uchaguzi wa mapema