Mwanamziki maaraufu wa nchini Kenya, Rosemary Wahu Kagwi maarufu kwa jina la ‘Wahuu’ alitangaza kuingia kwenye muziki wa injili mwaka mmoja uliopita na kuachana na muziki wa kidunia.

Wahuu amesema kuwa hajuti kufanya aina hiyo ya muziki akiwa na promoti wimbo wake mpya wa ‘Nifanane Nawe’ ambapo ameweka wazi kuhusu safari yake ya kwenye muziki wa injili

Aidha amesema kuwa anafuraha kubwa kwa mapokezi na kumekuwa na mrejesho chanya tangu atangaze kuwa anaingia kwenye muziki wa injili.

“Nimepokea nguvu kubwa kutoka kanisani na wanamziki wa injili  hivyo najisika vizuri kwani hata wasnii wasio wa injili pia wananipa nguvu,”amesema Wahuu

Akizungumzia kuhusu kuwahi kufanya muziki wa kidunia amesema kuwa hajutii kwa sababu ilikuwa moja ya sehemu ya safari yake.

Romelo Lukaku kuikosa Juventus FC
Video: Dudu baya afunguka kuhusu Mange Kimambi 'haniwezi'