Waislam katika kijiji cha Khaksabad nchini Pakistani, wamechanga fedha kusaidia ujenzi wa kanisa la majirani zao wakristo ikiwa ni miaka takribani sita tangu jumuiya hiyo ya Wakristo ipate pigo.

Kanisa hilo la Wakristo ambao wamekuwa wakipata misukosuko katika eneo hilo, lilisombwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali.

Daily Pakistan, imemkariri msemaji wa jumuiya ya waislamu wa kijiji hicho, Dilawar Hussain kuwa walifanya mkutano na kukubaliana kuwasaidia wenzao kujenga kanisa kwani wote wanamuabudu Mungu mmoja.

“Tulikubaliana kuhusu mradi huo katika mkutano wetu uliofanyika mwezi uliopita. Kanisa ni nyumba ya Mungu, ibada ni ndicho kitu muhimu. Tunamuabudu Mungu mmoja,” alisema Hussain.

Jumuiya hiyo ilieleza kuwa baada ya kutokea misukosuko na hali tete ya maelewano kwa kipindi cha nyuma, wamezimia kurejesha umoja wao na kuwaweka watu pamoja bila kujali imani zao.

Mwaka 2009, watu wasiojulikana walivamia nyumba za Wakristo na kuua watu 10. Pia watu saba walichomwa moto wakiwa hai ndani ya nyumba zao na makanisa yalivunjwa katika mji wa Gojra ambao uko karibu na kijiji hicho.

Video: 'Mbowe anawapigia simu Wabunge wakae kwenye chai badala ya kuingia Bungeni'-Mbunge Lusinde
Video: Profesa Lipumba apingwa kila kona. Ulimwengu ataka JK ashitakiwe - Magazeti Juni 15 - 2016