Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika ufunguzi wa Msikiti Mkuu mpya wa Paje, pamoja na ufunguzi huo, Dk. Mwinyi ameshiriki sala ya Ijumaa.

Katika hotuba yake Alhaj Dkt. Mwinyi amewasisitiza waumini kuzingatia maadili ya dini na kushiriki kikamilifu shughuli za misikiti ikiwa kutumia misikiti kama vituo vya ibada na kujitolea katika kusaidia kuboresha na kudumisha misikiti hiyo.

Aidha, amewashukuru waumini kwa kuchangia ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Paje huku akisisitiza umuhimu wa kuchangia kulingana na uwezo wa kila mmoja.

Alhaj Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo pia kutoa mchango wa shilingi milioni kumi kwa ajili ya huduma za msikiti katika eneo hilo tukio ambalo limefanyika hii leo Mei 12, 2023.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 13, 2023
Msako biashara ya maua yaliyoibwa makaburini waanza