Serikali imeagiza fedha kiasi cha Shilingi Millioni 800 zinazotokana na Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe ya Dhahabu zilizopo Kwenye akaunti ya kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime Mkoani Mara kutumika mara moja kabla ya Mwaka wa Fedha huku ikitekelezwa miradi ya Maendeleo ambayo ni kipaumbele kwa Wananachi.
 
Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali ya Kijiji Cha Nyamwaga katika ukumbi wa Shule ya Sekondari JK.
 
Amemuagiza Afisa mtendaji wa kijiji kuhakikisha anaitisha mkutano mara moja ili wananchi wapendekeze vipaumbele ili fedha hizo zilizopo kwenye akaunti ya kijiji ziweze kufanya
kazi ya maendeleo ya jamii.
 
“Nyie katika shule ya sekondari mnataja changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa Mabweni, Madarasa, Uzio wakati kwenye akaunti ya kijiji zipo fedha nyingi hamtaki kuzitumia sasa naagizza mara moja zitumike na kwa usahihi,” amesema Waitara.
 
Aidha Naibu waziri amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho kuhakikisha anapita katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa uchimbaji wa dhahabu Acacia North Mara na kuangalia fedha hizo zimefanya miradi ipi huku akikagua na kujiridhisha ili fedha hizo ziweze kuwasaidia Wananchi na siyo kutafunwa na baadhi ya vioingozi
 
Hata hivyo, Waitara amesema kuwa changamoto zilizosomwa mbele yake likiwemo suala la upungufu wa mabweni, madarasa na uzio katika shule ya Sekondari JK Nyerere sasa zitatuliwe mara moja na kuelekeza kuhusu uanzishwaji wa kidato cha tano na sita lazima kianze mara moja shuleni hapo.

Halmashauri ya Tarime Vijijini kujengwa Nyamwaga
Ramaphosa akemea mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni Afrika Kusini