Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(chadema) ameingilia kati mgogoro wa kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro kwa kumtaka Makonda kutoa uthibitisho wa tuhuma za rushwa dhidi ya kamanda huyo.

Aidha, Mwita amesema vitendo vya Makonda kutoa matamko ya hovyo kunajenga chuki dhidi ya makundi mbalimbali na kwamba anatakiwa atambue nafasi aliyonayo ni ya kuteuliwa na ipo siku hatakuwepo kwenye nafasi hiyo.

Ni ajabu kuona kijana mdogo kama yule anamtuhumu mtu aliyemzidi Weledi, Cheo, Umri na kila kitu,kwa sababu tu yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa. kama ni kweli alikataa kuchukua hizo hela ni kwanini hakuchukua hatua kwa kuwataja waliotaka kumpa hela? alihoji Waitara.

Hata hivyo Waitara amesema anachokifanya Makonda ni kujenga chuki kwa watumishi wa umma, wafanya biashara ndogndogo (wamachinga), wauza samaki na bodaboda.

Mbunge huyo alisema maeneo yote alikopita Makonda kufanya ziara,naye atapita ili kuwaaeleza wananchi kwamba mkuu huyo wa mkoa alikuwa akifanya siasa na si vinginevyo.

Video: Alichosema Magufuli kuhusu bomba la TAZAMA kupunguza uwezo wa kusafirisha mafuta
Antonio Conte Aomba Msaada Wa Mashabiki