Zaidi ya watu 65,000 wamefanya maandamano jana Okinawa nchini Japan kushinikiza wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo baada ya Komando mmoja wa jeshi a marekani kuhusishwa na tukio la kumbaka na kumuua mwanamke mmoja wa nchini humo.

Waandamanaji hao wenye hasira walivalia mavazi meusi kuashiria maombolezi pamoja na mabango yenye jumbe mbalimbali wakitaka Serikali ya nchi hiyo kufanya mabadiliko katika makubaliano ya ushirika wa ulinzi kati yake na jeshi la Marekani.

Makubaliano ya kiulinzi na kiusalama ndiyo yanayolipa ruhusa jeshi la Marekani kuendelea kukaa katika ardhi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Associated Press, mwili wa mwanamke huyo ulikutwa mwezi uliopita na uchunguzi ulibaini kuwa mwanajeshi huyo wa Marekani ndiye aliyeutelekeza. Hata hivyo, katika hati ya mashtaka, kosa la mauaji halikuorodheshwa.

Gavana wa Okinawa, Takeshi Onaga amesema kuwa anajutia uamuzi wa makubaliano hayo ya kiusalama kwani tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 1995, na waliapa kutoruhusu kujirudia.

Video: Wabunge Upinzani watoka Bungeni wakiwa wamejifunga plasta mdomoni
TFF Waushangaa Uongozi Wa Stand Utd Kampuni