Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko Rasmi ya Matunda, Mbogamboga na Samaki wabichi wametoa siku 14 kwa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhakikisha magari ya mizigo yanashusha bidhaa hizo kwenye soko rasmi la bonanza na sio mahali pengine.

Tamko hilo limetolewa na Katibu wa Soko la Tambukareli, Said Muumba ambapo amesema kuwa tangu mwaka 2009 halmashauri ya jiji la Dodoma lilizuia magari kushusha bidhaa za Samaki wabichi, Matunda na Mboga katika maeneo mbalimbali kama vile soko la Majengo lakini bado matangazo na matamko hayo yamepuuzwa na wafanyabishara wa bidhaa hizo.

Amesema kuwa baada ya siku 14 kumalizika bila kufanyiwa kazi kwa tamko hilo wafanyabiashara hao watahamishia biashara zao katikati ya Mji kwenye eneo la Uhindini hususani barabara inayotoka Nunge kuelekea eneo la Jamatini

Aidha, kwa upande wake mwenyekiti wa soko la Bonanza, Goha Magwai amesema kuwa kutolewa kwa tamko hilo haimaanishi wanajaribu au kutishia mamlaka husika.

Hata hivyo, Kutolewa kwa tamko hilo kumekuja mara baada ya wafanyabiashara hao kulalamika kuwa kumekuwa na utekelezaji mbovu wa matamko na matangazo yanayotolewa halmashauri ya Jiji la Dodoma tangu mwaka 2009 hadi mwaka huu 2019.

 

RC Songwe aagiza mwenye kitambulisho asisumbuliwe
Mangula atua Njombe, anena kuhusu mauaji, 'Msijichukulie sheria mikononi'