Wajasiriamali wadogo wameiomba serikali kuwatafutia muwekezaji atakaewaletea mashine za kutengeneza vifungashio pamoja na lebo ilikuweza kupunguza usumbufu wanaoupata.

Hayo yamesemwa na Anneth Kivuyo mjasiriamali alipokuwa akiongea katika semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na shirika la uthibiti wa Viwango(TBS) kwa kushirikiana na SIDO ambapo amesema kuwa changamoto ya vifungashio inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza soko la bidhaa za hapa nchini kwa sababu vifungashio havipo kwenye ubora unao kubalika.

Amesema kuwa Tanzania inabidhaa nzuri na zenye ubora lakini shida kubwa inayosumbua ni vifungashio hivyo aliihitaji serikali ijitahidi kupata muwekezaji atakaye saidia kuondoa tatizo hilo.

“Vifungashio bora vyakuvutia vitasaidia bidhaa zetu ziwe kwenye viwango vyenye ubora , serikali itushulikie tuwe na mtu atakaye wekeza mashine za lebo na kutengeneza vifungashio kama wenzetu wa nchi jirani kwani kwasasa tunaagiza nchi za nje na vinavyokuja pia vinakuwa vichache havitoshelezi mahitaji,“amesema anneth

Kwa upande wake mkurugenzi wa TBS, Jabir Abdi amesema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wachakataji wa bidhaa za ngozi lakini pia huo ni muendelezo wa kuhakikisha wanapata elimu sahihi itakayo wasaidia kufikia viwango vya kitaifa ili waweze kuuza bidhaa zao sio tu hapa nchini pia waweze kuuza nje ya nchi.

Hata hivyo, amefafanua kuwa wanatoa elimu hiyo pia ili waweze kupata alama za ubora pamoja na kuwawezesha kufikia malengo yao, kitu pekee kitakacho wawezesha wajasiriamali kufikia malengo ni kufuata sheria ya kufika viwango vya kitaifa.

Kilimanjaro yazizima, Waziri aliyefukuzwa na JPM ataja mambo 10 'yanayomtesa'
Watu waishio mijini watahadharishwa kuhusu Afya zao