Wanawake wajawazito wameshauriwa kupima angalau mara mbili kwa kutumia mashine ya Ultrasound ili waweze kujua maendeleo ya mtoto awapo tumboni.

Wito huo umetolewa na Daktari Deusi Kitapondya wa Chuo Kikuu cha Sayansi  Muhimbili ambapo amesema kupima kwa kutumia mashine ya Ultrasound kuna umuhimu mkubwa hasa kwa wanawake wajawazito na watu wanaopata ajali.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema mashine ya Ultrasound inarahisisha huduma hospitalini, lakini wakalalamikia madhara yatokanayo na mashine hizo.

Akijibu malalamiko hayo Daktari Kitapondya amesema mashine ya Ultrasound haina madhara yoyote na kusema hiyo ni imani potofu zilizopo kwenye jamii.

Hata hivyo, wananchi wameshauriwa kuondokana na dhana potofu juu ya matumizi ya mashine ya Ultrasound na badala yake kupima kwa kutumia mashine hiyo kwa sababu haina madhara yeyote.

Video: Itazame video ya Bonta 'Beautfull' akiwa na Nikki Wa Pili
Daktari wa Argentina aweka wazi hali ya Aguero

Comments

comments