Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewasisitiza wakinamama wajawazito kujitokeza kupata huduma za kiafya katika vituo mbalimbali vya afya Mkoani humo ili kujiepusha na madhara yanayojitokeza wakati wa kujifungua na kuwaasa kuachana na tamaduni za kujifungulia nyumbani kwani huduma zao ni bure.

Amesema kuwa sera ya afya ya mwaka 2007 inaelekeza kuwa makundi maalum wakiwemo wazee, walemavu, wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanapata huduma za kiafya bila ya malipo hivyo kuwataka watumishi katika vituo vya afya kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kutolewa bure.

Wangabo amesema hayo alipokuwa akikabidhi vitanda 55 ambavyo kati ya hivyo vitanda 20 ni vya kujifungulia na vitanda 35 vya kulalia wagonjwa vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 47, vilivyotolewa na Shirka lisilo la kiserikali Association of Rear Blood Donors (ARDB), na vimetawanywa katika vituo vya afya 9, Zahanati moja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.

“Nitoe wito kwa kina mama wote mnaotoka maeneo jirani na vituo vilivyotajwa, wanaofikia muda wa kuanza Kliniki au wanaofikia muda wa kuanza kujifungua wajitokeze na kufika katika vituo hivyo na kuachana na utamaduni wa kujifungulia majumbani,” Alisisitiza.

Awali kabla ya Kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dk. Boniface Kasululu alibainisha kuwa mahitaji ya chini vitanda katika vituo vya serikali kwa Mkoa ni 1008 na vilivyopo ni vitanda 564 ambavyo ni sawa na asilimia 56 na kisha kueleza sababu za upungufu huo.

“Upungufu huu unachangiwa na ufinyu wa majengo ya kutolea huduma, kwamba eneo ni dogo kiasi kwamba unakosa nafasi ya kuweka vitanda hivyo, lakini kwa msaada wa serikali kuvipa fedha vituo vitano vya afya mkoani kwetu kwaajili ya upanuzi na kuwezesha kupanua huduma hizi tunawaomba wadau wengine waweze kujitokeza kutupa ushirikiano na kuweza kuweka vuitanda vya kutosha katika vituo hivyo,” Amesema.

Wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, mratibu wa mradi wa ARBD Samwel Mwangi amesema kuwa shirikia hilo linawakilisha makundi ya damu ambayo ni A Negative, B Negative, AB Negative na O Negative leney wanachama 93 ndani ya Mkoa wa Rukwa wenye makundi ya damu mabyo hayapatikani kwa urahisi.

“ili kusaidiana na kutoa huduma kwa wananchi wake ARBD pamoja na shughuli nyinen ni kuhamasisha jamii kujitolea damu na kuhamasisha kinamama wajawazito kuhudhuria Kliniki kwa muda muafaka na kuwahamasisha kinamama hawa kuwapeleka watoto wao kuanza chanjo mpaka wanapomaliza chanjo” Ameongeza.

Magazeti ya Tanzania leo Februari 1, 2018
Aymeric Laporte avunja rekodi Man City