Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Walimu – CWT, Mkoa wa Dodoma, Clement Mahemba amesema kitendo kilichofanywa na baadhi wa wajumbe wa kamati tendaji kinakiuka katiba na kanuni za chama.

Mahemba ameyasema hayo huku Viongozi wa chama hicho wakiwemo mwenyeviti waastaafu wakidai kitendo cha kumsimamisha katibu mkuu wa CWT, Japheth Maganga kilichofanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji pia kinavunja katiba na kanuni za CWT.

Amesema, “kikao cha kamati tendaji kinazo taratibu rasmi na mialiko rasmi ya mwenyekiti lakini wamefanya uhubi wa kuendesha kikao chini ya mti na kuja maadhimio ambayo hanaya msingi mimi niwasahauri kama wanajambo lao wasubiri vikao rasmi.”amesema

Mapema hivi karibuni, baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya chama hicho walikutana jijini Dodoma na kufanya kikao kilichoazimia kumsimamisha katibu huyo kujihusisha na shughuli zote za CWT na nafasi yake kukaimiwa na Naibu Katibu Mkuu.

Mkude amuweka njia panda Kocha Simba SC
Wanandoa waingia matatizoni wakiwa Hotelini