Hewa inaendelea kuwa nzito mjini Dodoma ambako Tanzania nzima imetega sikio kujua nani ni nani kati ya watano waliopelekwa mbele ya NEC.

Taarifa kutoka mjini humo tulizozipata jioni hii zinaeleza kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kinaendelea huku baadhi ya wajumbe wa wakiwa wamekisusia kikao hicho. Mmoja kati ya wajumbe hao ni Dr. Emmanuel Nchimbi ambaye tangu jana usiku aliweka wazi kutoridhishwa na uamuzi wa Kamati Kuu.
Wajumbe hao wameshinikiza kuwa majina yote yarudishwe tena ili ufanyike uchaguzi upya wa kuyapata majina matano.

Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa chanzo cha kuaminika, mwenyekiti wa chama hicho, rais Jakaya Kikwete aliingia ukumbini na kupokelewa na wimbo wa ‘tunaimani na Lowassa’, ulioimbwa na baadhi ya wajumbe huku wakipiga makofi. Kikwete aliwaunga mkono kwa kupiga makofi hadi wimbo huo ulipokwisha na kutoa tamko rasmi kama mwenyekiti.

“Haijawahi kutokea…. haijawahi kutokea,” alisikika rais Kikwete.

Hata hivyo, Kikwete alisisitiza msimamo wake kuwa majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ndiyo yatakayopigiwa kura katika kikao hicho na si vinginevyo. Aliwataka wajumbe hao kuwa watulivu na kama wana hoja waziwasilishe hoja zao kwa utulivu na hekima.

Baada ya kauli hizo, mwenyekiti huyo aliwataka waandishi wa habari kuondoka ukumbini hapo ili kazi ya kikao hicho iendelee.

Kwa upande wa nje ya ukumbi huo, bado inaripotiwa kuwa hali ya usalama imeimarishwa vikali lakini polisi wamejitahidi pia kuwa wavumilivu hata wanapokuwa ‘provoked’ na wapambe katika hali ambayo haijaleta madhara, wakiangalia kwa kina kila sekunde ya tukio lisilete madhara yoyote.

Dodoma: Magufuli Ashinda Kwa Kishindo Kugombea Urais CCM
Membe Akanusha Kuhusika na Aliyekamatwa na Fedha Dodoma