Watu wanane wanashikiliwa na jeshi la Polisi nchini Nigeria kwa madai ya kutumia matairi chakavu kuchuna ngozi ya ng’ombe, mtindo unaofahamika kwa jina la “Cow canda” katika lahaja za kienyeji.

Taarifa ya Mamlaka ya Usalama na Ubora wa Chakula imesema washtakiwa hao (wanaume wawili na wanawake sita), walikamatwa wakiwa mafichoni nyuma ya machinjio eneo la Abuko Juni 21, 2022.

“Operesheni hii iliendeshwa kwa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usalama na Ubora wa Chakula na Polisi, ambao walikuwa wakifanya kazi kwa taarifa kutoka kwa raia wema,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema watu hao huchoma mipira ya matairi na yanaposhika moto huwekwa juu ya Ng’ombe aliyechinjwa ambaye huvimba mwili na kisha kuvuta ngozi yake kama njia ya mkato ya uchunaji ngozi.

Utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo umeonyesha kuwa kemikali ya polycyclic aromatiki hydrocarbons (PAH) na metali nzito ambazo hupatikana kwenye makombo ya mpira ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira.

“Mamlaka inaendelea na azimio lake lisilogawanyika la kuwabana wafanyabiashara wa chakula wasiotii sheria, na zoezi hili litakukuwa na mafanikio iwapo umma utaunga mkono,” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, tayari Mamlaka hiyo  ya Usalama na Ubora wa Chakula imewataka wananchi kutoa malalamiko yao kwa simu namba 1299 iwapo wataona tatizo lolote linalohusiana na uvunjwaji wa sheria na chakula ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

"Msinilinganishe na Michael Jackson" - Chris Brown
TAMISEMI kuongeza uwezo huduma kwa wateja