Makamu wapili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah ametoa wiki mbili kwa wakandarasi ambao hawajaanza kutekeleza miaradi ya maendeleo kuanza mara moja kazi za ujenzi wa miradi hiyo na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Makamu wapili wa rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah amelitoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mikoa miwili ya Unguja .

Katika ziara hiyo Makamu wapili wa rasi anaonesha kutoridhishwa na mradi wa Tangi la Maji safi na salama unatekelezwa bumbwini mkoa wa kaskazini Unguja.

Akikagua miradi ya ujezi wa hospital za wilaya na majengo ya Skuli, Makamu wa Pili wa rais ameridhishwa na kazi inayofanywa na wakandarasi waliokabidhiwa kazi hizo,

Katika hatua nyengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaataka wakala wa majengo Zanzibar (ZBA) kuhakikisha majengo ya Hospitali na Skuli yanakuwa na viwango bora na yenye kudumu kwa muda mrefu ili kunakisi fedha iliyotolewa na Serikali.

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud na mkuu wa mkoa wa kusini Rashid Hadidi Rashidi wakaahidi kuwasimamia wakandarasi ili kuona miradi hiyo mbali ya kukamilika kwa wakati bali inakuwa na ubora kwa mujibu wa makubaliano.

Katika Ziara hiyo makamu wapili wa rais amekagua eneo linalotarajiwa kujengwa Tangi la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni moja lililopo Bumbwini, ujenzi wa Hospital za wilaya Pangatupu, kivunge, kitogani pamoja na Mwera Pongwe na ujenzi wa skuli ya Elimu Mjumuisho Jendele pamoja na Ujenzi wa skuli ya Maandalizi ya Unguja Ukuu.

Majaliwa - Watanzania tushikamane kuipa thamani Tanzanite
Sijaridhishwa na hali ya Utekelezaji wa miradi Nzega - Dkt. Grace