Wakandarasi wa ujenzi wanaotarajia kuomba kazi kupitia Mradi wa kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji  Nchini Tanzania (TACTIC), wametembelea miradi inayotarajia kujengwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Wakandarasi hao, wametembelea miradi inayotarajia kujengwa katika kipindi cha awamu ya Kwanza kwa lengo la kuitambua na kuona uhalisia katika kipindi cha utekelezaji kabla ya kuomba zabuni (Pre bid visting).

Barabara zilizotembelewa na zinazotarajiwa kujengwa ni ile ya Wafipa -Kagera yenye urefu wa Km 2.43 ikiwemo Ujenzi wa daraja la Mto Luiche , na  barabara ya Bangwe-Burega-Ujiji, yenye urefu wa Kilometa 7.1.

Miradi mingine iliyotembelewa na  inayotarajiwa kujengwa ni  Mitalo ya Maji ya Bangwe,  Burega, Rutale, Mlole, Bushabani, Mji Mwema na Mtalo wa maji wa Katonyaga.

Aidha miradi mingine inayotarajia kujengwa katika Mradi ya kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji  Nchini Tanzania (TACTIC)  katika awamu ya Kwanza na ya pili ni pamoja na  Ujenzi wa Kisasa soko  la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, na Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Kilometa 7.

Esther atoa siri iliyompandisha cheo kazini
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 25, 2023