Timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeanza mazoezi kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Ligi hiyo imesimama kwa muda tangu mwisho wa mwezi uliopita na itaendelea tena mwanzoni mwa mwezi ujao.

Lengo la Shirikisho la soka nchini TFF kusimamisha ligi hiyo ni kupisha mechi za kimataifa za timu ya taifa, Taifa Stars pamoja na Kilimanjaro Stars ambayo kwa sasa ipo nchini Ethiopia kushiriki michuano ya Chalenji.

Akizungumza na mpanduka.blogspot.com msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru alisema wameamua kuanza mazoezi na watakuwa wakijifua ufukweni jijini Dar es salaam na kisha kurejea tena nyumbani Morogoro.

“Tumeamua kuanza mazoezi kwa kuwa hatuna wachezaji wengi wanaocheza katika timu za Taifa,”alisema Kifaru.

Zanzibar Heroes Wapotea Tena Ethiopia
Wafanyakazi Wa Maduka Ya Uchumi Supermarket Walalamikia Kuzulumiwa Stahiki Zao