Wakristo wa kikatoliki katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamefanya maandamano katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo kupinga ufisadi uliokithiri na kudai kuwa wanakerwa na ukiukaji wa sheria kwa kutowaadhibu wahalifu na kudorora kwa mfumo mzima wa sheria nchini humo.

Wameitisha maandamano hayo ya amani kufuatia kupotea kwa dola milioni 15 kutoka benki ya taifa ya DRC na kuwekwa katika benki ya biashara kabla ya kutoweka kabisa.

Licha ya kilio cha umma ambao uliwataka wahusika wachukuliwe hatua, Rais Tshisekedi wala mahakama hawajatoa maelezo ya kutosha kwa umma juu ya sakata hiyo.

Wakatoliki hao wanasema wanakataa mtindo wa kutotokomeza rushwa uliotawala tawala zilizopita.

Maandamano hayo ambayo yameitishwa na Kamati ya Katoliki ya Walei ambao wamewataka raia wa kongo kwa ujumla kuingia mitaani kupiga ufisadi na ukosefu wahaki za kisheria.

Walei ambao ni wakristo wa kawaida katika jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo wanaaminiwa kuwa ndio waliomshinikiza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kuacha azma yake ya kugombea muhula wa tatu madarakani.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Walei kuitisha maandamano chini ya utawala wa rais wa sasa Felix Tshiseledi.

Awali Gavana wa mji wa Kinshasa Gentiny Ngobila , pamoja na kamati ya uratibu ya Walei (CLC) walikubaliana kusitisha maandamano hayo mjini Kinshasa ili kuzuwia, yasifanyika siku Oktoba 19 Jumamosi ambayo ni siku ya ilipofanyika operation Kin Bopeto

Hata hivyo maandamano hayo yaliendelea katika maeneo mengine ya nchi kama ilivyopangwa.

Aidha, kamati ya Walei wa Kikatoliki DRC (CLC) imevipongeza vyama vya kisiasa, makundi ya raia pia mashirika yasiyo ya kiserikali waliopaza sauti zao kuunga mkono maandamano hayo.

Katika taarifa yake CLC imewataka watu “kutojihusisha na aina yoyote ya ghasia, kuchoma magurudumu, na kuweka vizuizi vya barabarani, kutotumia lugha ya matusi, kutorusha mawe na vitu vingine au kufanya uporaji wowote wa mali”.wakati wa maandamano hayo.

Wanasema wanataka kutumia kusanyiko hilo kama,”mfano wa kutumia uhuru kwa uwajibikaji ili kuijenga jamii ambayo ni bora kuishi “.

 

Upelelezi kesi ya aliyemuua na kumchoma moto mke wake yakamilika
Wanachuo wavalishwa mabox kukomesha udanganyifu wa mtihani