Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka kweye kiwanda cha muziki wa bongo fleva, Webiro Wassira maarufu Wakazi amedhihirisha kuchukizwa na vita inayoendelea kwenye tasnia ya muziki hasa ya wasanii wakubwa nchini ambao wamepata nafasi ya kufanya matamasha mbali mbali nje ya Nchi.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter Wakazi amebainisha hilo kwa kuandika ”nasikitishwa sana kuona watu walio karibu na wasanii wetu wakubwa  wanashiriki kukejeli jitihada za wasanii wengine ni kama wametumwa, narudia tena, Tanzania hatutifikia level za wa Naija kama tutaendeleza ushindani usipokuwa na tija baina yetu, alafu pia kama uko juu USIJISAHAU”.

Wakazi ameandika hayo kufuatia kukithiri kwa kwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu walio karibu na wasanii hao, ambao wamekuwa wakiitumia mitandao yao ya kijamii kubeza maendeleo ya matamasha ya wasanii wengine.

Aidha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram wakazi ameongeza kwa kuandika ”Wote bado tuna safari ndefu, sasa tunachekana kwa lipi, ni kweli hatua tumezidiana, ila hakuna aliyefika nchi ya ahadi.

nipo ughaibuni naona jinsi, Wizkid anajaza show, na Tiwa Savage anakuja kum-support, na Wizkid akiwa hana show anakwenda kwenye show ya Burna Boy…..na alienda hadi kwenye show ya Davido, SISI TUNACHEKANA.

Music fans are very fickle….hasa hawa wa huku ughaibuni. Ni muhimu kuwapa Expirience ya maana ili wawe loyalists…. tupende tusipende, sisi muziki wetu bado, na pengine sababu sio kutokana na mapungufu yetu, ila we are not doing ourselves a favor kwa kuleta ushindani na uswahili usio na tija.

mwenye sikio na asikie”. ameandika Wakazi, ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 19, 2021
Machinga Dar waongezewa siku 12