Wakazi wa Kimara, Dar es salaa. hasa eneo la kitunda, wamekuwa na kilio cha muda mrefu kutokana na kukumbwa na adha ya ukosefu wa maji ya kutosha katika baadhi ya maeneo kwa takribani miaka sita sasa.

Licha ya kuwepo kwa mikakati  mbalimbali ya serikali kutekeleza sera yake ya maji, kumwezesha kila mwananchi anaondokana na uhaba wa maji nchini, lakini bado idadi kubwa hainufaiki na huduma hizo katika maeneo mbalimbali ya Kimara.

Katika jiji la Dar es Salaam, eneo kubwa linalopata maji linahudumiwa na kampuni ya Dawasco ambayo ipo chini ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka, Dar es Salaam, Dawasa.

Vyombo vya habari vimefika katika kata ya Saranga, Mtaa wa Kimara Matangini mabomba yaliyowekwa kwenye baadhi ya nyumba yakiwa kama mapambo kwa kukosa maji kwa kipindi kirefu.


CUF waishukia CCM
Mwana FA, Darassa ‘watoana nduki’ YouTube