Wakenya waishio ughaibuni wanatarajiwa kupiga kura katika vituo vilivyoandaliwa huku jumla ya idadi ya waliojisajili ikiwa ni wapiga kura 10,443.

Uchaguzi wa leo unaoendelea Nchini Kenya umeandaliwa katika balozi 18, za Kenya zilizopo Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Qatar, Marekani, Uingereza, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu, na Canada.

Wakenya wanaoishi Tanzania watapiga kura katika vituo vitatu, viwili Jijini Dar es Salaam na kimoja Mjini Arusha.

Kituo cha Dar es Salaam kina jumla ya wapiga kura 496 waliosajiliwa, huku kituo cha arusha kikiwa na idadi ya waoiga kura 410

Maafisa wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), iliandaa zoezi la kuwaelimisha wapiga kura Agosti 7, 2022, kwenye ubalozi wa Arusha eneo la Uzunguni.

Hali kadhalika maafisa wa IEBC walitoa mafunzo kwa wapiga kura Juba ambako kuna Ubalozi wa Kenya Nchini Sudani Kusini.

Wengi waikimbia polio wiki ya unyonyeshaji
Watu 20 wafariki Dunia, 15 wajeruhiwa ajalini