Wakenya walioonekana kukerwa na wingi wa safari za nje za rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta wameanzisha ‘zengwe’  kwenye mtandao wa Twitter.

Watumiaji hao wa mtandao wa Twitter nchini humo wameanza kampeni ya kumkaribisha Kenyatta nchini kwao kama walivyofanya kuwakaribisha viongozi wakubwa waliowahi kuitembelea Kenya.

Kenyatta amefanya ziara 43 nje ya nchi kwa muda aliokuwa madarakani idadi ambayo inaonekana kumzidi mtangulizi wake, Mwai Kibaki aliyefanya ziara 33 kwa kipindi cha miaka kumi aliyokaa madarakani.

Karibu

Wakenya wanalinganisha kurejea kwa rais Kenyatta kutoka Afrika Kusini na ziara waliyofanya viongonzi wengine nchini humo ambao walikuwa wakikaribishwa kwa hashtag zilizokuwa maarufu kama #ObamaInKenya #PopeInKenya. Hivyo, wao wametengeneza hashtag ya #KenyataInKenya.

 

Ndoa Ya Yanga Na Andrey Coutinho Yavunjika Rasmi
Pale Uwanja Wa Soka Unapogeuka Msitu Wa Vita