Wakili, Albert Msando amekabidhi fedha shil. milioni tano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikiwa ni kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kulipa deni aliloahidi kumlipia mwanamke mmoja aliyekuwa amefiwa na mama yake mzazi.

Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwaona majeruhi wa ajali ya moto uliosababishwa na kupinduka kwa Lori la mafuta ya Petroli iliyotokea mkoani Morogoro Agosti 10 mwaka huu.

Aidha, akiwa Hospitalini hapo, alikutana na mwanamke mmoja aliyedai ni mkazi wa Morogoro ambaye alikuwa amefiwa na mama yake mzazi hospitalini hapo na kutakiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni tano.

Rais Magufuli aliagiza mwanamke huyo aruhusiwe kuondoka na mwili, huku akiahidi fedha hiyo angelipa yeye mwenyewe pia alimkabidhi mwanamke huyo kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya matumizi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema kuwa rais Magufuli  aliahidi kutoa fedha hizo baada ya mwanamke huyo kumlilia kuwa amefiwa na mama yake na hana msaada wowote.

Naye wakili Msando amesema kuwa alichangisha fedha hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram akihamasisha wananchi kulipa deni hilo.

Askofu Dkt. Shoo achaguliwa tena kuongoza Kanisa la KKKT
Video: Mawakili 15 wamwekea Tundu Lissu pingamizi | Uchaguzi Serikali za mitaa Novemba 24