Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Sambi anadaiwa kutohudhuria siku ya pili ya kesi yake ya uhaini, baada ya mawakili wake kudai kuwa hawana hakikisho kwamba atahukumiwa kwa haki.

Sambi, (64), ambaye ni mpinzani Mkuu wa Rais wa sasa wa Comoro, Azali Assoumani, anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na madai ya uuzaji wa hati za kusafiria za Comoro.

Mmoja wa mawakili hao, Mahamoudou Ahamada amesema, “Tuliondoka kwenye kikao kwa sababu hatukuwa na hakikisho la kesi ya haki,” huku wakili mwingine Jan Fermon, akisema “Sambi hatahudhuria tena kesi hiyo, inayotarajiwa kumalizika wiki hii.”

Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Sambi akitoka kuhudhuria kesi. Picha ya AFP.

Timu ya utetezi, imedai kuwa rais wa mahakama ya usalama inayomjaribu Sambi inapaswa kujiondoa kwa kuwa hapo awali aliketi kwenye jopo lililoamua kumfungulia mashtaka kiongozi huyo wa zamani lakini ombi lao lilikataliwa huku hakimu akisema hana ufahamu wowote kuhusu uhalali wa kesi hiyo.

Mwendesha Mashtaka katika kesi hiyo, Ali Mohamed Djounaid, amesema hukumu ingetangazwa kabla ya hii leo Novemba 24, 2022 bila kujali kama rais huyo wa zamani alihudhuria mahakamani au la.

Ahmed Abdallah Sambi, ambaye aliongoza visiwa hivyo vidogo vya Bahari ya Hindi kati ya 2006 na 2011, tayari ametumia miaka minne gerezani, licha ya sheria kuweka kizuizini kabla ya kesi kuzidi miezi minane.

Polisi: Hakuna dalili za kupungua kwa uhalifu
Nigeria yazindua noti mpya, Serikali yafunguka