Wakili wa kimataifa aliyepewa kazi ya kumwakilisha mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amezuiwa kuingia nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la the Monitor nchini humo limeripoti kuwa Robert Amsterdam ameorodheshwa kama mtu ambaye hatakiwi kuingia nchini Uganda.

Aidha, Wakili huyo alikuwa miongoni mwa mawakili waliokuwa wameorodheshwa kumtetea, Kyagulanyi katika kesi ambapo ameshtakiwa uhaini.

Jukumu la Amsterdam lilikuwa kufanya masuala ya kiufundi, kutoa ushauri na pia kusaidia katika kufanya utafiti na jinsi kesi hiyo inavyoendeshwa.

Hata hivyo, Wakili huyo ambaye ni raia wa Canada lakini huendesha shughuli zake kupitia kampuni ya Amsterdam & Partners yenye Ofisi zake Washington na London.

Unai Emery aanza kupata changamoto Arsenal
Birdman amuomba radhi Lil Wayne hadharani