Shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema kuwa mpaka sasa, wakimbizi wapatao 1200 wameingia nchini Tanzania. huku ikiaminika kwamba kuna wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

Limesema kuwa maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wameacha makazi yao huku mapigano makali dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yakiendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu.

Aidha, wakimbizi hao wamekuwa wakiingia nchini Tanzania kwa kutumia Ziwa Tanganyika, huku wakiwa wamechoka na baadhi wakiwa katika hali mbaya ya kiafya.

“Wakimbizi wanakuja kwa kwa kutumia boti, awali raia kutoka Congo walikuwa wanakuja kupitia Burundi kwa miguu, hiyo ndio tofauti na wakimbizi wa sasa, wanapokelewa na serikali na UNHCR, na mashirika mengine, tunawapa huduma zote za kibinadamu, wanapokelewa hapa, baadae wanaenda katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,” amesema Joan Allison mwakilisha wa UNHCR nchini Tanzania.

Hata hivyo, amesema kuwa wimbi la wakimbizi, limeongeza changamoto ya upatikanaji wa malazi, maji na hata huduma za choo, huku wengine wakiwa wanalala nje.

Video: Familia ya Lissu yajilipua, Udanganyifu watawala mtihani kidato cha nne
Putin: Hatima ya Wasyria iko mikononi mwao