Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua mpango wa Ruzuku ya Mbolea utakaowawezesha wakulima kupata mbolea kwa bei nafuu katika msimu wa kilimo wa mwaka ujao.

Uzinduzi huo leo umefanyika hii leo Agosti 8, 2022 katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane), ambayo yanafanyika katika uwanja wa John Mwakangale Mkoani Mbeya

Katika uzinduzi huo, Waziri wa Kilimo Hussen Bashe amesema mpango wa Ruzuku ya Mbolea unalenga kuwaondolea mzigo wakulima ambao umekuwa ni changamoto inayowakabili kwa muda mrefu katika shughuli zao za Kilimo.

Kutokana na mpango huo wa rukuzu unafanya bei ya mbolea ya DAP itauzwa Shilingi 70, 000 kutoka Shilingi 131,000 ya awali huku mbolea ya urea ikiuzwa Shilingi 70,000 kutoka Shilingi 124,734.

Aidha, katika hatua nyingine Bashe amewataka wadau wa maendeleo wanaotoa fedha katika sekta ya kilimo kusitisha utoaji huo kwenye miradi inayohusisha mafunzo na kujenga uwezo na badala yake zielekezwe kwenye miradi ya utatuzi wa changamoto za Kilimo nchini.

Amesema, “Niwaombee wadau wa maendeleo wasitelekeze mradi wowote wa kilimo bila kupata maelekezo ya Wizara ya Kilimo, tunataka wajue fedha wanazotoa zinaenda kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta na si katika mafunzo wezeshi.”

UN yaonesha wasiwasi ongezeko la ghasia Gaza
Serikali yasema haitavumilia ukatili, biashara ya Binadamu