Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote zilizopo mijini kuhakikisha wanawapatia wakulima wa mbogamboga maeneo ya wazi ili wayatumie katika kilimo

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene.

Simbachawene ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki, ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro Agosti 8, 2022.

Amesema, yapo maeneo mengi ya wazi ambayo hayatumiki na kwamba ni vizuri iwapo watawapatia wakulima wa mbogamboga ili waweze kuyatumia katika kilimo cha mjini kitakachowasaidia kuwaingizia kipato.

Kwa upande wao baadhi ya Viongozi, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe pamoja na wadau mbalimbali wa kilimo wamesema sehemu hizo za wazi zitawanufaisha vijana wanaoishi mjini na kujitengenezea ajira.

Azirai baada ya kugundua mkewe ni mmiliki wa nyumba waliyopanga
NHC yakusudia kumwaga ajira kwa Watanzania