Shirika la Chakula Duniani (FAO) linalotekeleza mradi wa kurejesha hali kwa Wakulima waliopatwa na majanga mbalimbali kwa kushirirkiana na Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, lipo katika hatua za mwisho kukamilisha mradi huo ulioanza tangu Mwaka 2017, unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu huku mradi huo ukionekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Mratibu wa Mradi huo, Amon Lugeiyamu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Kampeni ya Lishe na Mafunzo ya usindikaji.
 
Amesema kuwa, FAO Kupitia Halmashauri ya Wilaya Missenyi chini ya Timu ya wataalamu kutoka katika Idara ya Kilimo na Maendeleo ya jamii pamoja na kitengo kinachoshughulikia masuala ya lishe na Udumavu, mpaka sasa wamefanikiwa kuwajengea uwezo Wakulima kupitia semina na mafunzo mbalimbali, kugawa Vipando, Mbegu, Kuku na Vifaranga vya Samaki, Kutoa Elimu ya Lishe kwa Vijiji vinne, Kutekeleza Kampeni ya Lishe na Usindikaji kwa Vijiji Vinne vinavyolengwa na mradi huo.
 
Aidha, kwa Wilaya ya Misenyi tayari FAO wametekeleza kwa mafanikio makubwa mradi huo kwa kuzifikia Kaya za wakulima zipatazo 709 ndani ya Vijiji (5) vya Minziro, Karagala, Kikono, Nkerenge na Nyankere, ambapo wanufaika wa mradi huo ni pamoja na Vikundi vya Kijamii, akina mama, Wajasiliamali, Wafugaji, na Wakulima kwa jumla yake ni Vikundi 20.
 
  • Bandari Mpya yajengwa Muleba
 
  • Wizara ya Kilimo kuja na Sheria ya kumtetea Mkulima
 
  • Prof. Mbarawa azitaka mamlaka za maji kujitegemea
 
Hata hivyo, mradi kama huo pia unatekelezwa katika halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba Vijijini, Kyerwa na Muleba hivyo kufanya jumla ya halmashauri (5) ndani ya Mkoa wa Kagera.
Simba yafufua matumaini ya robo fainali, yaichakaza Al Ahly
Serikali yaweka mazingira mazuri ya uwekezaji

Comments

comments