Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imewahakikisha kuwapatia mikopo wakulima wa Zao la Karafuu visiwani Zanzibar katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika wakulima hao.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga wakati akitoa mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu visiwani Zanzibar katika Kikao cha Wadau wa Karafuu kilichokuwa kinafanyika mjini Unguja.

Amesema kuwa Serikali inatambua changamoto wanazokutana nazo wakulima nchini hivyo uanzishwaji wa TADB unalenga kutekeleza hatua mbalimbali zikilenga kuharakisha  mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo ikiwemo uendelezaji wa zao la karafuu ambalo ni zao kuu la biashara visiwani Zanzibar.

“Tunatambua kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliweka Mkakati  Maalum wa miaka 10 (2011 -2021) wa kuongeza uzalishaji, usafirishaji, ubora na tija wa zao la karafuu kwa kutambua hilo Benki inakuja kuongeza kasi juhudi hizi za Serikali,” amesema Assenga.

Hata hivyo ameongeza kuwa kwa kutambua juhudi za SMZ zao la karafuu lilipewa kipaumbele cha pekee  miongoni mwa minyororo ya thamani ya kwanza kuanza kupatiwa mikopo na Benki hiyo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali nchini.

 

Msuva anga'ara tena ufungaji bora
Trump kutoa hotuba yake falme za kiarabu