Taasisi  ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), imewaonyawakulima juu ya tabia ya kupanda mbegu zinazoingizwa nchinikinyemela kwa kuwa hizo zina madhara makubwa,

Akizungumza wa  ukaguzi wa mwishoni mwa wiki kwenye maghala ya kuhifadhia na maduka ya kuuzia mbegu hizo katika mikoa ya Mbeya na Songwe.Ofisa Mfawidhi wa TOSCI Nyanda za Juu Kusini, Peter Nassari, amesema madhara ya wakulima kutumiambegu zisizothibitishwa ubora ni makubwa kuliko serikali kukosa kodi ya uingizwaji wa mbegu hizo.

Nassari amesema mbali na madhara kiafya na kwenye mavuno, pia uingizwaji wa mbegu hizo kinyemelauna athari za kiuchumi kwa taifa kutokana na kukosa kodi. Amesema endapo uzalishaji utaporomoka kutokana na matumizi ya mbegu hizo pia uchumi utazorota.

“Sheria inataka mkulima atumie mbegu ambazo zimethibitishwa ubora na TOSCI. Sasa kitendo chawatu kuingiza mbegu na kuanza kuzitumia bila kuthibitishwa ni kosa. Lakini mbegu ambazo wanaingizani zile zile ambazo zinazalishwa hapa nchini,”amesema Nassari.

Naye Mdhibiti wa Ubora wa Mbegu kutoka taasisi hiyo, Salehe Kombo, amewataka wakulima kuhakikisha mbegu wanazonunua zina nembo ya TOSCI ambayo inaashiria kuwa imethibitishwa ubora.

Amewataka wafanyabiashara pia kuacha kuuza mbegu ambazo hazijathibitishwa na taasisi hiyo kwamaelezo kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria na endapo watakamatwa kuna adhabu kali ambazo zimeainishwa.

Baadhi ya wazalishaji wa mbegu wamesema kuna matatizo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokeaikiwamo mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huwa yakitokea wakulima wanakuwa na walakini nambegu zao.

Dkt. Ndungulile ayageukia makampuni ya simu
Rais Magufuli ateua Kamishna wa Maadili