Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka  Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya za Dodoma kukamilisha miradi yote kwa wakati  kabla ya kukamilika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambao utafikia tamati ifikapo Juni 30, 2023.

Senyamule ametoa maagizo hayo wakati alipofanya kikao kazi na viongozi wa Halmshauri za Wilaya na Mji za Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi yake.

Amesema, “tumebakiwa na takribani mwezi mmoja wa kukamilisha miradi yote kwa muda uliowekwa tunatakiwa kufanya haraka na kwa weledi kabla ya Juni 30, na sisi aliotuteua kumsaidia tunatakiwa tufanye kazi kwa nguvu ili kumuunga mkono.”

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.

“Lazima tufanye ubunifu ili majengo ya miradi tuliyopatiwa fedha yakamilike kwa wakati na niwasisitize muwalipe mafundi fedha zao kwa wakati kwasababu ukishamlipa fundi atafanya kazi kwa weledi, tununue vifaa kwa wakati, ili kuondoa ucheleweshaji ikiwa ni pamoja na kuwakwamisha kuendelea na kazi zao kwa mujibu wa mpango kazi uliopo,” Amesema Senyamule,

Aidha, amewaasa viongozi hao wa Wilaya kufanya uchambuzi wa vyanzo vyote ambavyo havikukusanya mapato na kuvitafutia namna nzuri ya kukusanya mapato na amebainisha kuwa Mkoa umekusanya mapato kwa asilimia 76 huku asilimia 24 pekee zikisali.

Young Africans hawatanii fainali ya CAF
Kocha Minziro aipa kongole Geita Gold