Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurungenzi wanne wa Halmashauri nne nchini kwa matumizi mabaya ya ofisi pamoja  na kuwahonga maofisa wa ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) waliowaandikia hati safi kufunika uchafu wa hesbau zao.

Akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Simbachawene aliwataja wakurugenzi hao kuwa ni Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkoani Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara,   Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.

Kadhalika, Waziri huyo ametangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani  Mbeya, Halima Ajali kwa tuhuma za kuwatumia watoto wake katika kazi za Halmashauri hiyo na kuwalipa posho.

Simbachawene ameagiza Mamlaka husika kuwachukulia hatua haraka watumishi wa ofisi ya CAG waliotajwa kupokea rushwa na kushirikiana na wakurugenzi hao kufanya udanganyifu na kuandika hati safi kwa halmashauri zilizostahili hati chafu, kitendo kinachopeleka hata Bunge kujadili ripoti ambayo imechakachuliwa.

 

Wema Sepetu atoa ya Moyoni kuhusu ujauzito wake
The Game aahidi kumsaidia Kanye West $10,000,000 kwa masharti haya