Sera ya kubana matumizi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima imewaathiri Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) na vigogo wengine katika ngazi za mikoa kwenye safari zao zilizozoeleka kuelekea Bungeni kama wageni wakati Bunge la Bajeti.

Serikali ya Awamu ya Tano imeeleza kuwa watumishi hao hawatakuwa na fursa ya kuingia Bungeni katika awamu hii na badala yake wametakiwa kubaki katika vituo vyao vya kazi kuwatumikia wananchi.

Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene amesema kuwa Mawaziri wa Wizara husika wataambatana na maafisa wasiozidi kumi wa Wizara hizo tofauti na ilivyo kuwa awali.

“Hii yote ni kwenda na dhamira ya Rais ya kubana matumizi ya Serikali zamani alikuwa akija Mkuu wa Mkoa, RAS (Katibu Tawala), na mchumi na hawa wote wanakuwa na magari kati ya moja hadi matatu, safari hii wamekuja watumishi wa wizara, wakuu wa mikoa nilimalizana nao kule Dar es Salaam wabaki mikoani kwao wafanye kazi zao,” Waziri Simbachawene anakaririwa.

Kutokana na uamuzi huo wa Serikali, Mji wa Dodoma umeshuhudia utofauti mkubwa wa mahurudhurio ya vigogo mjini hapo na kusababisha biashara nyingi zilizozoeleka kushamiri wakati huu zikikosa wateja.

Mpango wa CIA kuadhimisha Kifo cha Osama kwa njia hii wapingwa
Wabunge wa CCM wapinga kwa sauti Bunge kuoneshwa Live, Ukawa waja na mbinu mbadala