Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya nchini washirikiane na Madiwani katika halmashauri zao kufanya tathmini ya mali zote zinazomilikwa na halmashauri vikiwemo vibanda vya biashara ili kujiridhisha kama viwango vinavyotozwa vinalingana na hali halisi ya uchumi kwa sasa.

Amesema kuwa licha ya tathmini hiyo kuwawezesha kufahamu viwango vinavyotozwa, pia itasaidia halmashauri kubaini watu wa kati ambao wanawatoza wafanyabiashara fedha nyingi na kuilipa halmashauri fedha kiduchu.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Mji wa Nzega pamoja na Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani humo mkoani Tabora.

Aidha, Majaliwa amebaini kuwa kuna baadhi ya wamiliki wa awali wa vibanda waliviuza kwa wafanyabiashara wengine kwa bei kubwa bila ya kuishirikisha halmashauri na ilivyotaka kuvichukua ili wafanyabiashara waendelee kuwa wapangaji kwa lengo la kuondoa mtu wa kati, ndipo ulipoibuka mgogoro wa umiliki wa vibanda hivyo.

Hata hivyo, Majaliwa amezishauri halmashauri zinazomiliki vibanda vya biashara hususani kwenye maeneo yenye migogoro watumie leseni za biasahara zinazofanyakazi kwa kuzitambua na kuingia mikataba na wamiliki wake ili kuondoa uwepo wa mtu wa kati.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 18, 2018
Madiwani wanne wa Chadema wasimamishwa