Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 6 akiwemo Mabula Mabula mkazi wa mji mpya kwa tuhuma za kuwakamata wanawake nyakati za usiku, kuwapora mali, kuwafanyia vitendo vya kikatili kuwalawiti na kuwapiga picha za utupu.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei na kusema kukamatwa kwa mtuhumiwa Mabula ni kufuatia matukio kadhaa ya aina hiyo yaliyo ripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya mji huo.

Amesema Watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia mbinu ya kudanganya kuwa ni askari kisha kuwapeleka sehemu wasizozijua na kuwatishia silaha na kuwapora mali zao na kisha kuwapiga picha za utupu.

”Akifika anatoa kisu, anatoa mapanga anaanza kumfanyia vitendo ambavyo ndivyo sivyo na kumpiga pichaza utupu” amesema Ulrich.

Kamanda Matei amesema baada ya kupata taarifa, jeshi hilo kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa makosa ya mitandao pamoja na Kikosi cha kupambana na ujambazi wakafanikisha kupatikana kwao

Watuhumiwa hao walipohojiwa walidai kuwa wanafanya matukio hayo kwa lengo la kutafuta pesa.

Wizi wa mtandaoni wawatia mbaroni 3
Video: Kinondoni kwasasa iko shwari- Kamanda Murilo

Comments

comments