Wali nazi ni chakula cha kitamaduni ya Afrika, hivyo Taasisi ya Wali Nazi Food Festival kwa kushirikiana na Hoteli ya Ramada Resort Mbezi iliyopo jijini Dar es salaam, imeandaa tamasha la chakula aina ya wali nazi na vyakula mbalimbali vya kiafrika litakalofanyika Aprili 2, mwaka huu katika hoteli hiyo.

Tamasha hilo litahudhuriwa na mabolozi 30 kutoka mataifa mbalimbali duniani pamoja na wafanyabiashara 150 lengo likiwa kutangaza aina hiyo ya chakula maarufu inayopatikana na kupendwa na watanzania wengi.

Hivyo mwanzilishi wa shughuli hiyo, Hellena Kapango amesema amejipanga vyema kutangaza chakula hiko cha asili ya Afrika duniani kote na kusema kuwa huu ni mwanzo tuu, tamasha litakalo fanyika jumatatu ya pasaka litakuwa dogo huku tamasha kubwa limepangwa kufanyika kipindi cha sikukuu ya Iddi.

Mkurugenzi Mshirika wa Taasisi hiyo, Salum Kihemba amesema tamasha hilo ni la aina yake na kuwataka wananchi kushiriki katika tamasha hilo.

 

Amesema kuwa kiingilio katika tamasha hilo ni 200, 000 kwa mtu mzima na watoto chini ya miaka 14 watalipa shilingi 100,000, miziki, chakula na burudani mbalimbali zitapatikana kwa watoto na watu wazima.

Aidha Meneja Masoko Mwandamizi wa Hoteli ya Ramada Resort, Amina Kapya amesema wanawakaribisha watu wote kushiriki katika tamasha hilo.

 

 

 

Video: Prof. Lipumba anatumika, si yule tunayemfahamu- Maalim Seif
Video: Ujio mpya wa Ney wa Mitego ''Amsha Popo"

Comments

comments