Warembo 16, waliokuwa wanashiriki shindano la kumtafuta Miss Burundi wamejiondoa katika hatua ya fainali iliyopangwa kufanyika Julai 21, 2018 na kupelekea shindano hilo kuhairishwa mpaka Julai 28, mwaka huu.

Hali iliyopelekea nchi ya Burundi kuingiwa na hofu kubwa ya kupatikana kwa mlimbwende atakaye iwakalisha nchi hiyo kimataifa kwa mwaka 2018 katika mashindano yenye mlengo wa kuonyesha utamaduni, uweledi na urembo wa mwanamke wa Burundi.

Hata hivyo warembo hao wamefikia maamuzi hayo ya kususia shindano hilo kufuatia madai kuwa shindano la mwaka huu kumefanyika udanganyifu mkubwa upande wa zawadi itakayozawadiwa kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.

Ambapo waandaaji wa shindano hilo, Burundi Event hapo awali walitangaza washindi hao kujinyakulia gari, kiwanja chenye mita mraba 400 pamoja na hundi ya pesa taslimum, cha kushangaza ni kwamba walimbwende hao wanadai kuwa hakuna maandalizi yeyote ya zawadi hizo.

Aidha kufuatia mzozo huo wanakamati watano wa shindano hilo waliamua kuchukua uamuzi wa kujiudhulu.

Kitaeleweka ndani ya saa 48 zijazo
Eritrea, Ethiopia wamaliza rasmi vita, simu zaleta msisimko