Tume ya utumishi wa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari za umma nchini imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu ambao watabainika kufanya mapenzi na wanafunzi pamoja na utoro kazini.

Akizungumza na Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari zaidi ya 100 Wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya Mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa walimu Tanzania, Oliver Muhaiki amesema mojawapo ya kazi kubwa ya tume hiyo ni kusimamia maadili na wajibu wa walimu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa baadhi ya walimu nchini wamekuwa wanashindwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na wanafunzi na utoro kazini vitendo ambavyo amesema havipaswi kuvumiliwa na tume hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya walimu, Mektirisi Kapinga amesisitiza umuhimu wa walimu kufahamu Muundo wa tume hiyo inapokuwa inasimamia masuala yanayowahusu walimu.

Hata hivyo, imebainishwa kuwa uwepo wa tume hiyo ambayo ni maalumu tu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari za umma, kunawapa matumaini walimu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kutatuliwa changamoto zao.

 

 

JPM: Mimi ndivyo nilivyo
Tanzia: Mzee Kingunge afariki dunia