Walimu katika shule za Serikali nchini Sudan, wameingia rekodi ya mgomo wa tangu Novemba mwaka jana wakilalamikia mishahara midogo na kutolipwa ujira wao huku wakiishutumu Serikali ya kijeshi kwa kushindwa kuwekeza kwenye elimu na kutaka kurejeshwa kwa serikali ya kiraia.

Madai hayo yanakuja ikiwa ni kipindi kirefu tangu kuanza kwa mgomo huo, huku Waziri wa fedha wa Sudan akisema Serikali ya nchi hiyo imekidhi madai ya waalimu na wanachotakiwa kufanya ni kurejea kazini kutimiza wajibu wao.

Kituo cha Mafunzo cha Walimu nchini Sudan. Picha ya Sudan Relief Fund.

Shule za Sudan kwasasa hazina wanafunzi ambao ni kawaida kuonekana maeneo yote, na Walimu wanapinga madai ya Waziri huyo wakimtaka naye kushughulikia madai ya mishahara ambayo haikulipwa awali na ongezeko la mishahara.

Wanasema, wana wasiwasi kuhusu elimu ya wanafunzi na poromoko la kitaifa la watoto hao katika nyakati zijazo uraiani kwani litaharibu vizazi kadhaa na jamii huku wakisema Serikali inapaswa kufikiri kwa kina juu ya changamoto inayowakabili.

Program Mwanamke Kiongozi itumike kuibua vipaji: Waziri SMZ
Awaumbua ndugu wa mume waliomkejeli kisa hana mtoto