Walimu wa Shule ya Sekondari Magu Mkoani Mwanza wamechangia milioni 14 kwaajili ya ujenzi wa chumba cha darasa katika shule hiyo ili kukabiliana na upungufu wa madara ya kusomea wanafunzi.

Mkuu wa shule ya sekondari Magu, Mwalimu Sahani Bilaazah amebainisha wazo la kuchangia ujenzi huo lilitokana na ongezeko la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2019.

“Sisi walimu tumeamua na kwa imani tuliyonayo kwa serikali yetu ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli tunaonyesha njia kwa vitendo ili jamii ijitoe kuchangia shughuli za maendeleo hasa kwa ujenzi wa miundombinu hapa shuleni” Amesema Bilaazah

Amesema kuwa kwasasa hivi sasa shule inawanafunzi 1,320 na vyumba vya madarasa vilivyopo ni 14 kwa kidato cha kwaza hadi cha nne badala ya kuwa na vyumba 27 hivyo upungufu hadi sasa ni vyumba 13.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Mwlimu, Mwandu Michael ameeleza kuwa zoezi hilo ni shirikishi na hiari hivyo walimu walioridhia wanachangia kiasi cha Tsh 35,000 kila mwezi na mwalimu mkuu amechangia milioni moja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Lutengano Mwalwimba amesema kuwa ameridhishwa na uzalendo wa walimu hao, na tayari amesha muagiza Mhandisi wa ujenzi kufanya kazi bega kwa bega na kamati ya walimu unayosimamia ujenzi wa mradi huo.

 

Lugola aagiza iundwe tume ya uchunguzi, 'Haiwezekani mwananchi ateswe na Polisi'
JPM afanya uteuzi wa Mkurugenzi TEWW

Comments

comments