Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametengua nafasi za wakuu wa shule za msingi zaidi ya 30 pamoja na maafisa elimu kata 13 wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kutokana na kuzembea kazini na kusababisha wilaya kushuka kitaaluma.

Uamuzi huo ameutoa baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Tumaini Magesa kwenye kikao kazi alipokutana na watendaji wa serikali, na kutoridhishwa na kiwango cha ufaulu, huku akimuonya afisa elimu wa shule za msingi na utumishi kushindwa kuwachukulia hatua watumishi.

“Mkishindwa kusimamia walimu kufundisha tunawafuta, tunaweka wengine, ndani ya wiki mbili tatu nao tukiona wameshindwa tunafuta, na wenyewe tunaweka wengine hivyo hivyo mpaka mwisho, wakati huo tunawasubiri walimu wa sekondari na matokeo yao yakiwa ya hovyop nao tunafuta”, amesema Mnyeti.

Shule za wilaya hiyo zimeshindwa kufikia kiwango cha ufaulu wa wastani wa asilimia 50 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa mwaka 2017, na kitendo kilichomkera Mkuu wa Mkoa Mnyeti.

Kamati ya maadili kumhoji Ole Sendeka
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba aagiza wenye mimba kukamatwa

Comments

comments